MERIDIANBET WADONDOKA MAWASILIANO NA MAKUMBUSHO KUGAWA REFLECTORS KWA MADEREVA

 

Meridianbet kama ilivyo kawaida yao wanaendeleza utamaduni wao kurudisha kwenye jamii ambapo leo wamefika katika vituo vya Bajaji na Bodaboda mitaa ya Mawasiliano na Ubungo ambapo wamegawa Reflectors kwa madereva katika maeneo hayo.

Wabobezi hao kwenye michezo ya kubashiri walilenga zaidi kuhakikisha madereva wa magari na bodaboda wanafanya kazi zao katika usalama mkubwa wakati wakiwa kwenye majukumu yao ya kila siku.

Msimu mpya wa ligi mbalimbali barani ulaya nao umerejea rasmi na Meridianbet wanakuambia “MSIMU MPYA MZIGO WAKUTOSHA” kwa maana ya kwamba usiache kubashiri na kampuni hiyo yenye ODDS KUBWA

Mkuu wa kitengo cha Masoko kutoka kampuni ya Meridianbet Nancy Ingram alizungumza baada ya kufika maeneo hayo na kusema “Leo tumetoa vifaa vya usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda na bajaji ambavyo ni Reflectors, Tunajua thamani ya madereva wa bodaboda na bajaji katika safari zetu, ndio maana tumeona kutoa vifaa hivi vya usalama kwa madereva wetu.

Unafahamishwa kwa kipindi hiki ambacho ligi zimerejea na “MZIGO UPO WAKUTOSHA” Meridianbet wanakuambia Jackpot ipo palepale kupitia simu za vitochi *149*10# kwa shilingi 1000 tu.

Madereva Bajaji na Bodaboda katika maeneo hayo ya Mawasiliano na Makumbusho walizungumza kwa vipindi tofauti na kuonesha kufurahishwa na msaada huo ambao kampuni hiyo imeutoa kwao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post