SERIKALI YA INDIA YAFURAHISHWA USHIRIKIANO WAO NA TANZANIA KWENYE SEKTA YA MAJI

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akimkabidhi maua Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar wakati Waziri huyo wa India alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam leo Julai 7,2023.

****************

NA EMMANUEL MBATILO

Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India.

Akizungumza katika ziara hiyo leo Julai 7,2023 Jijini Dar es Salaam, Dkt. Jaishankar amesema suala la maji ni muhimu hivyo basi Serikali ya India inaipongeza Tanzania kwa kuhakikisha wananchi wake wanapata maji kwa uhakika.

Amesema wamejipanga kikamilifu kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha huduma muhimu ya majisafi inaboreshwa.

"Serikali ya India inatambua umuhimu wa huduma ya maji kwa kuwa ni hitaji la msingi na la uhakika kwa wananchi kwa ujumla". Amesema Dkt. Jaishankar.

Kwa upande wake Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameitaka DAWASA kuhakikisha kazi ya kuunganisha maji kwa wananchi wote wa Kibamba inatekelezwa kwa kasi ndani ya wiki moja ili kila mwananchi apate maji.

Pamoja na hayo ameipongeza Serikali ya India kwa jitihada kubwa ambazo wamekuwa wakizifanya za kuboresha huduma ya maji Tanzania.

Amesema kuwa kupitia Serikali ya India huduma ya maji mijini na vijijini imeimarika kwa kiasi kikubwa na kazi inaendelea ya kusambaza maji kwa kasi ili kufikia malengo yaliyopo.

"Kwa sasa upatikanaji wa maji kwa maeneo ya mijini imefikia asilimia 88 na vijijini imefikia asilimia 77, na kazi inaendelea ya kuimarisha huduma ili kufikia malengo ya Serikali," ameeleza.

Nae Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu ameipongeza Serikali ya India kwa uwekezaji mkubwa wanaoufanya nchini kwenye miradi ya majisafi, hii inasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya Majisafi kwa wananchi.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu kuhusu maendeleo ya tanki la kuhifadhi maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India wakati alipofanya ziara kutembelea mradi huo leo Julai 7,2023


Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw. Kiula Kingu kuhusu mkakati wa uusambazaji wa maji kwenye maeneo ambayo yatapata huduma kupitia tanki la kuhifadhi maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India wakati alipofanya ziara kutembelea mradi huo leo Julai 7,2023

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akimkabidhi zawadi ya picha Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar wakati Waziri huyo wa India alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam leo Julai 7,2023.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza wakati Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar alipofanya ziara kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar alipofanya ziara kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Albert Chalamila akizungumza wakati Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar alipofanya ziara kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India.

Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mhe.Issa Mtemvu akizungumza wakati Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar alipofanya ziara kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesoakizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Albert Chalamila wakati Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali ya India Dkt.Subrahmanyan Jaishankar alipofanya ziara kutembelea na kukagua Maendeleo ya tenki la Kuhifadhi Maji Kibamba Jijini Dar es Salaam, lenye ujazo wa lita milioni 6 lililojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post