CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR CHAANDAA MASHINDANO YA MICHEZO 'MAMBOSASA CUP'
Na  Abel Paul wa Jeshi la Polisi.

Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kimeandaa mashindano yatakayohusisha wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi lengo la mashindano hayo ni kuwaweka Pamoja wananchi na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na uhalifu hapa nchini.


Mkuu wa chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Dk. Lazaro Mambosasa amesema mashindano hayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu na yatahusisha michezo yote ambayo washiriki wake ni maofisa wanafunzi na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi kutoka katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam.

Ameongeza kuwa tayari maandalizi yamekwisha kamilika kwa asilimia mia hivyo amewakaribisha wananchi wa maeneo ya karibu na chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kufika kushuhudia mashindano hayo katika chuo hicho kilichopo wilaya ya Temeke maeneo ya Kurasini jijini Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post