AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI BAADA YA KUMUUA MAMA MKWE MADAI KASABABISHA MKEWE AONDOKE

Mussa Sagi (38) mkazi wa Kitongoji cha Kubiha Kijiji cha Bonchugu Kata ya Sedeko Wilaya ya Serengeti ambaye amemuua mama mkwe Ryoba Nyang’au (66) kwa kumchoma kisu akidai amechangia mke na watoto kuondoka,naye amekufa kufuatia kipigo kutoka kwa wananchi.

Tukio la Sagi kumuua mama mkwe wake limetokea leo Jumanne Mei 16,2023 saa 2.30 asubuhi katika Senta ya Bonchugu baada ya kumfuata kwenye mgahawa wake limethibitishwa na Polisi Wilayani hapa,uongozi wa Kijiji na Kata.


Sagi baada ya kutenda tukio hilo alikimbia na kujificha katika kichaka mpakani mwa Kijiji cha Bonchugu na Rwamchanga,hata hivyo kundi la wananchi wakiwa na silaha mbalimbali za jadi walifanikiwa kumpata na kuokolewa na Polisi wakati akishambuliwa,hata hivyo amefariki muda mfupi kabla ya kufikishwa hospitali ya Nyerere.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyerere Edgar Muganyizi amethibitisha kupokea mwili wa Mussa Sagi,”ni kweli mchana tulipokea mwili wa Ryoba Nyang’au ambaye inadaiwa ni mama mkwe wake,na jioni hii nimetaarifiwa kuwa mwili wake umeletwa na Polisi kwa ajili ya kuhifadhiwa,”amesema.


Chanzo - Antomatv Online

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post