TMFD , FAO WAZITAKA NGO's KUWA WADAU WA KUTUMIA MWONGOZO WA HIARI WA KUPUNGUZA UPOTEVU NA UHARIBIFU WA CHAKULA



Mwandishi wetu -Dar es salaam

Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisberies Development (TMFD) Bwana Edwin Soko amekutana na Afisa na Shirika la chakula na kilimo Duniani Bwana Omar Riego Penaruba kutoka Rome na kujadili kwa pamoja umuhimu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini Tanzania kutumia mwongozo wa hiari wa kupunguza upotevu na uharibifu wa chakula Nchini .


Bwana Soko amesema kuwa, kwa kuwa TMFD ipo karibu na vyombo vya habari hivyo itatumia sauti kuhamasisha umuhimu wa mwongozo huo kwenye kupunguza upotevu na uharibifu wa chakula Nchini.


" Pia tutahakikisha mashirika yanayofanya kazi katika sekta ya uvuvi yanaufahamu mwongozo huu wa FAO ili yaweze pia kutengeneza mipango mathubuti ya kuhamasisha jamii kuwa wadau wa kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi kwa kutumia mwongozo huu uliotolewa na FAO." Alisema Soko


Kwa upande wake afisa wa FAO Omar alisema kuwa masharika yasiyo ya Kiserikali ni wadau wakubwa wa uzuiaji wa upotevu wa mazao ya uvuvi Nchini hivyo itakuwa jambo jema kwa TMFD kusaidia mashirika mengine kuufahamu mwongozo huo.


Mazungumzo hayo yamefanyika leo Jijini Dar es salaam na TMFD itaanza mara moja kuunadi mwongozo huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments