NEC YAFANYA UTEUZI WA MADIWANI WATATU WANAWAKE WA VITI MAALUM


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imefanya uteuzi wa Madiwani watatu (3) Wanawake wa viti maalum kuziba nafasi zilizoachwa wazi katika Halmashauri tatu za Tanzania bara.


Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 86A (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 kikisomwa pamoja na kifungu cha 35 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 na kifungu cha 19 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288.


Taarifa ya Tume iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima, imesema Tume imefanya uteuzi huo katika kikao chake kilichofanyika tarehe 8 Mei, 2023 jijini Dodoma na kuteua Madiwani Wanawake Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).


Imewataja madiwani walioteuliwa kuwa ni Sina Jamaldin Nyanga wa Manispaa ya Lindi, Mary Muhjimy Kombe wa Wilaya ya Morogoro na Mashavu Juma Barakabitse wa Kigoma Ujiji.


Kailima amesema uteuzio huo umefanyika baada ya Tume kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa kwa mujibu wa kifungu cha 13 (1) cha sharia ya uchaguzi ya serikali za mitaa sura 292, akiitaarifu tume kuhusu uwepo wa nafasi wazi za madiwani wanawake wa viti maalum katika Halmashauri tatu za Tanzania bara.


Nafasi hizo zimetokana na vifo vya madiwani wanawake wa viti Maalum wa Kata husika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments