TET YAZINDUA MAABARA YA TEHAMA NA KUKABIDHI VIFAA VYA MRADI WA KLIC 2022


Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo tarehe 18/4/2023 imekabidhi vifaa vya kielektroniki kutoka nchini Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean e-learning Improvement Cooperation 2022) pamoja na uzinduzi wa maabara ya TEHAMA kwa shule ya Msingi Tegeta "A" ya jijini Dar es salaam.

KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na nchi ya Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia ya mtandao kwa walimu 20 wa shule ya msingi Tegeta A.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET , Dkt. Aneth Komba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya Elimu nchini ambapo ameeleza kuwa walimu katika shule hiyo wataweza kutekeleza kwa urahisi kazi ya ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya kieletroniki.

Dkt Komba amewataka walimu hao kuhakikisha wanaleta matokeo chanya ambayo yatasaidia katika uboreshaji wa elimu.

"Mkayatumie mafunzo vizuri na vifaa hivyo mlivyokabidhiwa kwa kuleta matokeo chanya na tuone ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa Tegeta A" ,Amesema Dkt.Komba.

Tukio hilo liliambatana na kukabidhi vishikwambi 20 kwa walimu walioshiriki programu ya mafunzo hayo.

Kwa upande wake , Mwalimu Mkuu wa shule ya Tegeta A Bwana. Alistides Ntakire ameshukuru kwa mafunzo hayo pamoja na vifaa vilivyotolewa ambapo amesema ana imani yataleta tija katika shule yake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Bwana Yassin Marijan ameshukuru kwa kuzinduliwa maabara hiyo ya TEHAMA na kukabidhiwa vifaa vyote huku akieleza kuwa atahakikisha vinatumika ipasavyo katika kuboresha elimu.

Vifaa vilivyokabihiwa ni pamoja na 'UPS 26,computure Monitor 25, system Unit 25,Wirless keyboard 35,projector moja, scanner moja,printer moja, wireless mouse 35, headphone 25, electric blackboard moja ,webcamera 26,digital podium moja,wired keyboard 25, ,wired mouse 25,speaker 26,adapter 49 na usb flash disk 50'



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments