MBUNGE UMMY AWAPA POLE WAATHIRIKA WA MVUA MAKORORA TANGA

MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya katikati akimuonyesha kitu Afisa Mazingira wa Jiji la Tanga  Kizito Mkwambi wakati alipofanya ziara  kuangalia athari za mafuriko iliyotokana na mvua 


MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya katikati akimsikiliza Afisa Mazingira wa Jiji la Tanga  Kizito Mkwambi kulia wakati alipofanya ziara  kuangalia athari za mafuriko iliyotokana na mvua 

 

 


Na Oscar Assenga,Tanga.

Mbunge wa Tanga Mhe Ummy Mwalimu leo tarehe 23/4/2023 akiambatana na Afisa Mazingira wa Jiji la Tanga,  Kizito Mkwambi amekagua baadhi ya miundombinu iliyoathirika na mafuriko jijini Tanga, ikiwemo eneo la Ziwani, Kata ya Usagara na Mzingani. 


Mhe Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya amelitaka Jiji na Tarura Wilaya ya Tanga kuangalia namna ya kuzibua mirefeji iliyoziba haraka ili kuondoa kero ya mafuriko eneo hilo na maeneo mengine ya Jiji.

Aidha Mhe Ummy ameeleza kuwa Suluhisho la kudumu la kuondoa kero sugu ya mafuriko eneo la Ziwani ni kutafuta fedha ili kuchimba mfereji wa kupitisha maji yanayotuama katika eneo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post