MGANGA WA JADI AFARIKI AKICHEPUKA NA MKE WA PASTA.... TALAKA YA FASTA YAZUA GUMZO


Pasta mmoja nchini Nigeria amemtaliki mke wake kwa madai ya kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mganga.

Pasta Joshua Ajagunigbala alivunja ndoa yake na Rita Ajagunigbala akimkashifu kwa kushiriki ufuska na mganga, Yaba Left.com imeripoti.

Kulingana na mtumishi wa Mungu, mganga huyo alikata roho alipokuwa akipakua asali ya mkewe katika hoteli moja eneo la Ikere-Ekiti mnamo Januari 2, 2023. 

Kisa hicho kilisababisha taharuki na kufanya majambazi kuharibu nyumba na kanisa la pasta huyo.

Ajagunigbala alilalamika kwamba kitendo cha mkewe kilisababisha kufungwa kwa kanisa hivyo haakuwa na hamu tena na ndoa yake na kuomba mahakama kuivunja kumpa haki ya kuwalea watoto wake.

Mkewe Ajagunigbala kwa upande wake alijibu mashtaka hayo, akikiri kuwa katika mahusiano na marehemu mganga huyo.

Alijiteta akisema uhusiano wake na mganga huyo ulitokana na kukosa kutunzwa na mume wake akiongeza kuwa yeye ndiye alikuwa ametwikwa majukumu ya kuwalewa wanao kwa kuwalisha na kuwalipia karo ya shule.

Alidai kwamba alikuwa na deni kubwa sana, ambalo marehemu alimsaidia kulilipa. 

Katika uamuzi wa mahakama, pasta Ajagunigbala aliagizwa kuwajibikia kikamilifu malezi ya wanao wawili wadogo kwani bado ni wachanga. 

Akitoa uamuzi huo, Rais wa korti hiyo alisema Joseph Oyedele alishikilia kwamba ndoa ya wawili hao haikuwa inatambuliwa kisheria hivyo wako huru kila mtu kuenda njia yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post