BILIONI 15 KUSAIDIA UHIFADHI NCHINI


Dar es Salaam, April 20, 2023

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Mohammed Mchengerwa na Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess, leo Dar es Salaam, wameshuhudia kusainiwa kwa Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Bilioni 15 (Euro milioni 6), Kusaidia Tanzania Kupambana na Wanyama Waharibifu katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania. 

Mkataba huo umetiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi na Dkt. Mike Falke, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani nchini (GIZ).

“Kusainiwa kwa mkataba huu ni ishawa kuwa Serikali imeanza na itaendelea kulipa uzito suala la uhufadhi na hasa kupunguza athari za wanyama waharibifu kama tembo kwa kushirikiana na wadau kama mnavyoona hapa leo,” alisema Waziri Mchengerwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post