JAMAA ASHANGAZA WATU AKITAFUNA KUKU MBICHI KABISA


Jamaa mmoja amewaduwaza watu baada ya kuonekana akirarua paja mbichi la kuku akiondoka katika duka la jumla.

Kama ilivyoripotiwa na Mirror, mwanaume huyo mwenye misuli alionekana akimla kuku moja kwa moja baada ya kumnunua katika duka hilo.

Mnunuzi aliyechanganyikiwa alichukua picha ikimuonyesha mlofa huyo bila viatu, akiwa amevalia fulana na kutafuna nyama mbichi. 

Picha hiyo ilipakiwa kwa Reddit ambapo watu wengi walibaki vinywa wazi.

Haya ni maoni ya watu kuhusu picha hiyo ya Daily Mail. 

"Kuku anaweza kuwa mbichi lakini kwa hakika jamaa amepikwa," mmoja aliandika. 

Mwingine akaongeza: "Jamani nani yuko karibu naye aweze kubaini endapo jamaa yuko sawa?' "Je, huyo ni kuku mbichi? Tafadhali niambie picha hiyo ni ya utani tu," mtu wa tatu alisema. 

"Hana muda wa kupoteza kuketi ale, kuvaa viatu, au kupika chakula chake. Ni wachache wanaoelewa mtindo huu mpya wa jamaa," mwingine alisema.

"Huyu atashikwa na salmonella," mwingine aliongeza. 

"Huyu apewe wiki nzima apumzishe akili kwake," mtu alisema. 

"Mtu anajaribu kabisa kutafuta ugonjwa kwa siku chache zijazo," mwingine aliandika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post