MWAKILISHI WA JIMBO LA MTAMBWE HABIB ALI MOHAMED AFARIKI DUNIA


Habib Ali Mohamed.

MWAKILISHI wa Jimbo la Mtambwe, visiwani Zanzibar, kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Habib Ali Mohamed, amefariki dunia, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Saiffe, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma ACT-Wazalendo, Salim Biman, Mohamed amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 3 Machi 2023.

“Chama cha ACT-Wazalendo kinatuma salamu za pole Kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, wananchi wa Mtambwe, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu Mohamed, kwa kuondokewa na kiongozi wetu, mwanafamilia na mpendwa wetu,” imesema taarifa ya Bimani.

Kupitia taarifa hiyo, Bimani amesema ratiba ya mazishi itatolewa baadae baada ya chama hicho kushauriana na famili ya marehemu Mohamed.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments