KAMATI YA BUNGE YAPITISHA MAOMBI YA BAJETI TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)


Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq akieleza jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa mwaka wa fedha 2023/24, Bungeni, Jijini Dodoma

Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakisoma taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa mwaka wa fedha 2023/24, Bungeni, Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa mwaka wa fedha 2023/24, Bungeni, Jijini Dodoma,


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akichangia jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) 2023/24, kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akieleza jambo wakati wa kikao hicho.


Sehemu ya Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia maelezo ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa mwaka wa fedha 2023/24, Bungeni, Jijini Dodoma


Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Thomas Malekela akiwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) 2023/24, kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma.



PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)



Na: Mwandishi Wetu - DODOMA



Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepitisha maombi ya bajeti ya mwaka 2023/24 ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Kikao cha kamati hiyo kimefanyika leo Machi 23, 2023 bungeni na kuongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Fatuma Toufiq ambao CMA iliongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.

Akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi, amesema Tume hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Idara ya Kazi ya Ofisi hiyo katika utatuzi wa migogoro ya kazi.

Awali, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu amesema dira ya Ofisi hiyo ni kuhakikisha inajenga jamii yenye mahusiano mema mahali pa kazi, nguvukazi shindani na maisha bora.

Katika taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya CMA kwa mwaka 2022/23, inaonesha Tume hiyo imesajili migogoro ya kikazi 12,570 ambapo migogoro 10,201 ilitatuliwa sawa na asilimia 81.2.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments