BENKI YA CRDB, ZFF NA SHERIA NGOWI WAINGIA MKATABA WA UDHAMINI WA JEZI ZA ZANZIBAR HEROES


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita (katikati waliosimama) akishuhudia utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na udhamini kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), kati ya Benki ya CRDB iliyowakilishwa na Afisa Mkuu wa Biashara, Boma Raballa (kulia) Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) lililowakilishwa na Rais wake, Abdullatif Ali Yassin (katikati) pamoja na Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi chini ya Sheria Ngowi mwenyewe (kushoto). Udhamini huo ni wa utengenezaji wa Jezi na Vifaa vya Michezo kwa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa muda wa miaka 5, na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), pamoja na Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi. Hafla ya kusaini mikataa hiyo imefanyika Machi 17, 2023 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Wengine pichani ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Hafidh Mohamed Ali (wapili kushoto waliosimama), Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Hussein Ahmada Vuai pamoja na Wanasheria.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na udhamini kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), kati ya Benki ya CRDB, Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) pamoja na Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi, iliyofanyika Machi 17, 2023 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.
Sehemu ya wageni waliohudhulia hafla hiyo wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita wakati akitoa hotuba yake.

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na udhamini kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), kati ya Benki ya CRDB, Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) pamoja na Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi, iliyofanyika Machi 17, 2023 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Abdullatif Ali Yassin akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na udhamini kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), kati ya Benki ya CRDB, Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) pamoja na Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi, iliyofanyika Machi 17, 2023 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.
Mbunifu wa Mitindo nchin na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi Brand, Sheria Ngowi akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na udhamini kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), kati ya Benki ya CRDB, Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) pamoja na Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi, iliyofanyika Machi 17, 2023 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.

Sehemu ya Wadau wakifatilia hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita na Ujumbe wa Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF).
Picha ya Pamoja na Viongozi wa Benki ya CRDB.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments