POLISI SHINYANGA WAKAMATA PIKIPIKI, BANGI, TV, MAFUTA YALIYOIBIWA MRADI RELI YA KISASA

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Leornad Nyandahu akionesha mali zilizokamatwa na Jeshi la Polisi 

Na Halima Khoya,Shinyanga.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata lita 302 za mafuta ya diesel katika maeneo tofauti ya mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), pikipiki 04 zilizokuwa zikitumika kufanyia uhalifu ,dawa za kulevya aina ya bangi kilo 22 mifuko mitatu ya saruji na magodoro 02.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Machi 20 2023, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Leornad Nyandahu amesema mali hizo zimekamatwa katika kipindi cha kuanzia tarehe 28,02,2023 hadi tarehe 20,03,2023 kupitia misako na doria kwenye maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga.

Nyandahu amesema Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata printer 01, kompyuta 01,TV 02,mbolea kilo 30,pamoja na battery 10 za magari ambazo ziliibiwa kwa vipindi na tofauti.

“Watuhumiwa 13 wamekamatwa na wapo mahabusu wakisubiri hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani”,amesema.

Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kuwasihi wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kutokomeza uhalifu na pia linaahidi kuzifanyia kazi taarifa mbalimbali za kihalifu zinazotolewa na wananchi kwa usiri mkubwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Leornad Nyandahu akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 20,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Leornad Nyandahu akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 20,2023.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Leornad Nyandahu akionesha mali zilizokamatwa na Jeshi la Polisi 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Leornad Nyandahu bangi iliyokamatwa na Jeshi la Polisi 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Leornad Nyandahu akionesha mali zilizokamatwa na Jeshi la Polisi 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Leornad Nyandahu akionesha mali zilizokamatwa na Jeshi la Polisi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments