KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA MKOA WA SHINYANGA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Katiba na Sheria imetembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga ambalo linaendelea kujengwa kwa lengo la kusogeza karibu huduma za kimashtaka karibu na wananchi.

Akitoa taarifa za ujenzi wa jengo hilo kwa kamati hiyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul amesema kuwa Septemba 26 mwaka 2022 Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliingia Mkataba na Mkandarasi Eliroi Construction kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga wenye thamani ya Bilioni 2.15 ikijumuisha ongezeko la Thamani VAT.

Gekul amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya muda wa miezi 8 ambapo ulianza kutekelezwa Novemba 22,2022 ambapo unatarajia kukamilika June 22 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 35.

Gekul ameongeza kuwa mpaka sasa mkandarasi amekwishalipwa fedha za awali kiasi cha shilingi milioni 323 kati ya bilioni 2.15 huku Mkandarasi Mshauri Mwelekezi wa mradi Water Institute Kawazulite maombi ya kulipwa kiasi cha shilingi milioni 335.5 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitalu ameishukuru Kamati hiyo kwa juhudi zake kubwa za kuipigania Ofisi hiyo ambapo kwa mwaka huu wa fedha unaondelea jumla ya mikoa sita imepatiwa fedha za ujenzi wa Ofisi ikiwa ni pamoja na Shinyanga,Geita,Manyara, Rukwa, Katavi na Njombe na kufanya idadi ya ofisi zinazojengwa kufikia kumi.

DPP Mwakitalu ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa huo Christine Mndeme kwa kuwapatia eneo la Kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo ambayo itasaidia na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii juu ya masuala ya Mashtaka ambapo amesema eneo hilo awali ilipewa taasisi nyingine.

DPP Mwakitalu amesema kuwa ujenzi huo utakapokamilika utarahisisha utaoaji wa huduma kwa jamii ambapo watumishi watakuwa na sehemu bora na mazingira rafiki ya utaoji wa huduma kwa wananchi.

Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi huo kampuni ya Eliroi Construction Bw Ngakuka Ngakuka amesema kuwa mradi huo umechelewa kufikia asilimia 50 mpaka sasa kutokana na kuchelewa kwa malipo ya awali sambamba hilo Ngakuka amesema kuwa licha ya kuraisi cheti cha malipo yanakwama kutoka kwa wakati 

Nao baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo Boniphace Butondo wamesema kuwa msukumo mdogo wa utoaji wa fedha unachangia kasi ndigo ya ujenzi wa majengo hayo ambayo yanapaswa kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Christine Mndeme ameahidi kamati hiyo kuwa atahakikisha anaisimamia kwa ukaribu ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na kuleta tija iliyokusudiwa ya utaoji wa huduma kwa jamii.

Mndeme ameishukuru serikali kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo kwani muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga huku akiongeza kwa  kuwa mradi huo unakwenda kubadili mandhari ya Mkoa wa Shinyanga

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (Mb)Florent Kyombo amemtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuwa muda aliyopewa mpaka sasa ni zaidi ya miezi minne mradi huo bado uko asilimia 35 ambapo alipaswa kuwa asilimia zaidi ya 50.

Kyombo amesema kuwa lengo la ujenzi wa Ofisi hizo ni kusogeza huduma karibu na wananchi hivyo usimamizi Madhubuti unapaswa kuwepo ili kuondoa mikwamo ya ujenzi huo isiyo kuwa na tija katika ujenzi huo

Aidha Kyombo ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itakayosaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Katiba na Sheria leo imefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Manispaa ya Shinyanga.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul akitoa taarifa za ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa kamati hiyo. 
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul akitoa taarifa za ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga kwa kamati hiyo.
Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa mradi huo kampuni ya Eliroi Construction Bw Ngakuka Ngakuka akizungumza katika ziara hiyo.
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga
Hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments