WEMBE ULIOSAHAULIKA TUMBONI WATOLEWA BAADA YA MIAKA 11Madaktari nchini Kenya wamemfanyia upasuaji Bi. Felister Namfua (36) na kutoa wembe wa upasuaji uliosahaulika ndani ya tumbo kwa muda wa miaka 11.


Bi Felister amekua akiishi na maumivu makali ya tumbo kwa miaka 11 akiamini kuwa ana vidonda vya tumbo (ulcers) na amekuwa akipata matibabu ya ugonjwa huo.

Tatizo hilo lilianza wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza katika hospitali ya Kitale Magharibi mwa Kenya.


Kadri miaka ilivyozidi kwende, aliendelea kupata maumivu makali, ndipo madaktari walipata shauku kuwa ugonjwa alionao ni mkubwa kuliko vidonda vya tumbo.Mume wa Felister Stephen Mungai ameomba vyombo vya usalama nchini humo kuchunguza madaktari wamliofanyia upasuaji mke wake huku akidai fidia kutokana na matatizo waliomsababishia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post