SERIKALI YAANZA KUANGALIA DHAMANA KESI ZA ULAWITI NA UBAKAJI


Na Mwandishi wetu, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum imeanza kuangalia uwezekano wa kuondoa dhamana kwenye makosa ya ulawiti na ubakaji ili kukomesha vitendo hivyo vilivyokithiri nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi ameyasema hayo bungeni leo Februari mosi, 2023 alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Judith Kapinga kwa niaba ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji serikali ina mkakati gani wa kurekebisha sheria ya ubakaji na ulawiti wa watoto ili kuwe na kifungu tofauti cha sheria.

Akijibu swali hilo, Mhe.Katambi amesema kukithiri kwa vitendo hivyo hakutokani na mapungufu kwenye sheria na kwamba uthibitishaji wa makosa ya jinai unatakiwa kufanyika bila kuacha shaka yeyote lakini ushahidi huharibiwa wakati wa upelelezi.

Naibu Waziri Katambi amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliona hilo na kuunda Tume maalum ya haki jinai.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments