MWANAFUNZI AMUUA KWA KISU MWALIMU WAKE


Mwanafunzi wa shule ya upili nchini Ufaransa amemuua kwa kumchoma kisu mwalimu mmoja raia wa Uhispaniaa katika shule moja katika mji wa Saint-Jean-de-Luz nchini Ufaransa.

Msemaji wa serikali ya Ufaransa Olivier VĂ©ran amethibitisha shambulio hilo la Jumatano ya leo na kusema mhusika ana umri wa miaka 16.

Polisi wamefika katika shule ya Saint-Thomas d'Aquin na mwendesha mashtaka wa eneo hilo, ambapo mwanafunzi huyo alikamatwa. Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kwamba mshambuliaji huyo aliingia darasani wakati mwalimu huyo wa Uhispania akitoa darasani na kumshambulia kwa kisu.

Mwalimu huyo anayekadiriwa kuwa na na umri wa miaka 50 alifariki kutokana na mshtuko wa moyo baada ya huduma za dharura kuwasili shuleni hapo, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Inasemekana mshambuliaji huyo alifunga mlango wa darasa na kumdunga kisu mwalimu huyo kifuani mwake.Waziri wa Elimu wa Ufaransa, Pap Ndiaye ameelekea mara moja shuleni hapo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post