WANANCHI KATAVI WAVUTIWA NA HATUA YA WIZARA YA AFYA KUELIMISHA SURUA KWA NJIA YA SINEMA

 


 
Na Elimu ya Afya kwa Umma.

Baadhi ya wananchi kutoka kata ya Majimoto Halmashauri  ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi wamepongeza  Wizara ya Afya kwa kuanza   zoezi la uelimishaji na uhamasishaji wa chanjo ya Ugonjwa wa Surua  kwa njia ya Sinema  katika Mkoa wa Katavi.

Wakizungumza mara baada 
kushuhudia uelimishaji kuhusu  madhara ya ugonjwa wa Surua na umuhimu wa Chanjo ya Surua, baadhi ya wananchi hao wamesema hatua hiyo itawasaidia kuwajengea uelewa zaidi umuhimu wa Chanjo na madhara yatokanayo na ugonjwa wa Surua.

Kwa upande wake mratibu wa uelimishaji huo kutoka Wizara ya Afya Simon Nzilibili amesema hatua hiyo ya uelimishaji kuhusu Surua mkoa wa Katavi itarahisisha kufikia wananchi wengi kwani muda wa jioni asilimia kubwa ya wananchi ni rahisi kupatikana baada ya kutoka kwenye shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo .

Ikumbukwe kuwa Wizara ya Afya imekuja na mikakati mbalimbali ya uelimishaji Surua ikiwemo kutumia magari ya Matangazo, lugha mama ,wasanii wa nyimbo za asili, viongozi wa dini, wazee wa kimila na watu mashuhuri, njia ya Sinema,mabango na vyombo vya habari pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kutokana na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa shirikishi na  kuwajali wananchi wake, Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu tayari ameshafanya ziara Mkoani Katavi ambapo Februari 24.2023 amezungumza na wananchi wa Majimoto katika Mkutano wa hadhara.

Hatua hii imekuja baada vifo 13 vitokanavyo na Surua kuripotiwa Mkoani Katavi ambapo Moja ya vyanzo ni wazazi kutokuwa na mwitikio wa kuwapeleka watoto vituo vya afya kupatiwa chanjo .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments