EWURA, PAU WARIDHISHWA NA MAENDELEO UJENZI WA MIUNDOMBINU MRADI WA  EACOP, TANGA


Meneja mradi wa EACOP Chongoleni Tanga, Mathieu Faget, akitoa maelezo ya mradi kwa Wajumbe wa Bodi ya PAU, menejimenti ya EWURA na PAU, walipotembelea mradi huo Januari 30,2023 Chongoleani Tanga.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Petroli Uganda, Bw. Ernest Rubondo, akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Petroli EWURA, Bw. Gerald Maganga, katika jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo, Chongoleani Tanga.


Picha ya pamoja

............................

Na.Mwandishi Wetu-TANGA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Mamlaka ya Petroli Uganda (PAU), imeridhishwa na maendeleo ya awali ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu katika mradi bomba la mafuta EACOP, katika eneo la Chongoleani Tanga.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi wa Petroli EWURA, Bw. Gerald Maganga alisema: “Tumeridhishwa na hatua za awali katika uandaaji wa ujenzi wa mradi huu, tumeona maeneo mbalimbali yakiandaliwa kwaajili ya kujenga matanki na miundombinu mingine kwa kuzingatia ushirikishwaji wa wazawa katika kufanya kazi mbalimbali”

Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Petroli Uganda (PAU), Bw. Ernest Rubondo, amepongeza hatua iliyofikiwa, kwani inaonesha matumaini makubwa katika maendeleo ya ujenzi wa bomba hilo la mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

Inakadiriwa kuwa takribani mapipa 216,000 ya mafuta ghafi yatasafirishwa kwenye bomba hilo kwa siku, kutoka Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani mkoani Tanga, nchini Tanzania ambapo yatajengwa Matanki ya kuhifadhia mafuta, kabla ya kupakiwa kwenye meli kuuzwa katika masoko ya nje.

Bw. Maganga alimalizia kwa kutoa mwito kwa watanzania, kuendelea kujiandikisha katika kanzi data ya EWURA, ili waweze kutoa huduma katika miradi ya gesi na mafuta nchini ikiwemo mradi wa bomba la mafuta la EACOP.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments