BIBI HARUSI AANGUKA AKIKATA VIUNO KWENYE SHEREHE YA HARUSI YAKE

 

Bibi harusi aliyekuwa na furaha kupita kiasi alijikwaa na kuanguka chini alipokuwa akisakata densi kwenye sherehe ya harusi yake.

Katika video, bibi harusi huyo aliyevalia mavazi ya kupendeza anaonekana akiimba kwa furaha wimbo wa Ghana huku wageni wakishangilia.

Mwanamke huyo anaonyeshwa akicheza wimbo wa kitamaduni na kuvalia viatu vyenye visigino virefu kwa hafla hiyo. 

Wakati alipokuwa akinengua kiuno, mwanamke mwingine aliotokea jukwaani kumnyunyizia pesa.

Katika harakati hiyo, bibi harusi huyo aliyejawa na furaha alipata nguvu ya hata kusakata densi zaidi. 

Wakati wa densi yake ya kipekee, bibi harusi huyo alijikwaa na kuanguka chini, na kusababisha tafrani kwenye sherehe yake. 

Video hiyo, iliyopakiwa na Prissy Ekua Adiepena Hemans kwenye akaunti yake ya Facebook, ilivutia maoni mseto ya wanamtandao ambao walichekeshwa na video hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post