ATUPWA JELA MIAKA 50 BAADA YA KUMLAWITI MKEWE NA KUMUWEKEA CHUMVI, KISU, PILIPILI NA SUPER GLUE 'Gundi' SEHEMU ZA SIRI


James Kifo Muriuki, mwanaume aliyemshambulia mkewe amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela na Mahakama ya Chuka Law nchini Kenya.

Akiwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Njoki Kahara, mtuhumiwa huyo alipatikana na hatia ya kumlawiti mkewe na kumsababishia madhara makubwa.

James Kifo Muriuki aligonga vichwa vya habari nchini humo baada ya kumdhuru mkewe mnamo Mei 16, 2020.

Inadaiwa wiku ya tukio, Mwanaume huyo alimvuta mkewe hadi mto Kathita huko Marimanti usiku, na kumwamuru avue nguo na kusema/kutaja Wanaume wote aliolala nao alipokuwa akiishi Nairobi.

Ndipo inadaiwa mwanaume huyo alianza kumpiga kabla ya kunyunyizia pilipili, chumvi na gundi (Super Glue) kwenye sehemu zake za siri. Kisha alitumia kisu kusukuma mchanganyiko huo kwenye sehemu ya siri ya mwathiriwa.

Mnamo Mei 21, 2020, Mwanaume huyo alikamatwa katika maficho yake huko Kaningo katika Kaunti ya Kitui na timu ya maafisa wa DCI kutoka kitengo cha Uhalifu Maalum, DCI Tseikuru na DCI kutoka Kaunti Ndogo ya Tharaka Kusini.

Mwanaume huyo alikuwa amejificha kwenye nyumba ya James Murogi ambaye aliaminika kufanya shughuli za uganga, kesi hiyo imekuwa ikiendelea tangu wakati huo huku James akikana kutenda kosa hilo.







Via: Citizen Digital

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments