TUME YA UCHAGUZI YAKUBALI RUFAA ZA WAGOMBEA UDIWANI ACT WAZALENDO KATA YA MWAMALILI, DUNDA NA MAJOHE


Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha leo tarehe 6 Desemba, 2022 imepitia, imechambua na kuzifanyia uamuzi rufaa tatu za wagombea Udiwani zilizowasilishwa kwa Tume. Rufaa hizo zimewasilishwa kufuatia baadhi ya wagombea Udiwani kutoridhika na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi kufuatia mapingamizi yaliyoweka katika zoezi la uteuzi uliofanyika tarehe 30 Novemba, 2022 katika Kata 12 za Tanzania Bara.


Katika kikao hicho, Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa Tatu za wagombea Udiwani na kutoa maamuzi yafuatayo:-


i. Imekubali rufaa ya Ndugu Joseph Yunja Machiya kupitia ACT-WAZALENDO na kumrejesha katika orodha ya wagombea wa Udiwani katika Kata ya Mwamalili, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.


ii. Imekubali rufaa ya Ndugu Vitali Mathias Maembe kupitia ACT-WAZALENDO na kumrejesha katika orodha ya wagombea wa Udiwani katika Kata ya Dunda, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.


iii. Imekubali rufaa ya Ndugu Samwel Azaria Mnyellah kupitia NCCR-MAGEUZI na kumrejesha katika orodha ya wagombea wa Udiwani katika Kata ya Majohe, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post