ALIYEMFUMANIA MKEWE NA KUUA MCHEPUKO ATUPWA JELA MIAKA 15


Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, imemhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani mkazi wa Kata ya Chikonji, Manispaa ya Lindi, mkoani humo, Omari Salum Hamisi (21), baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mke wake, Nasra Selemani (20), aliyemfuma na mwanaume mwingine.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Dkt. Eliamini Issaya Laitaika, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mwenyewe kukiri kosa la kuua lililokuwa linamkabili.

Baada ya kutiwa hatiani,wakili aliyekuwa anamtetea mshitakiwa huyo, Happynes Sabatho,akaiomba Mahakama kumpa adhabu iliyo nafuu mteja wake,ikizingatiwa bado ni kijana anaehitaji kulitumikia Taifa lake,na amekaa ndani (Rumande) kwa muda mrefu hivyo amejutia kosa lake.

Jaji Laitaika alimuuliza mwanasheria wa Serikali Yahaya Gumbo iwapo ana kumbukumbu ya makosa ya zamani kwa mshitakiwa, akajibu hana huku akiiomba Mahakama kumpa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia ya kuuwa binaadamu wenzao ili kupunguza vitendo hivyo ndani ya mkoa wa Lindi na vitongoji vyake.

Imeelezwa kuwa Hamis alitekeleza mauaji hayo baada ya kutomkuta nyumbani mke wake na alipomfuatilia alimkuta na mwanaume aliyekimbia mara baada ya kuwakaribia, na alipomuhoji mke aliyekuwa nae, alishindwa kujitetea ndipo ugomvi ulipoanza na kumkata kisu tumboni na kusababisha kifo.


CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post