WATAHINIWA 2194 WAFUTIWA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA, SHULE 24 ZAFUNGIWA KWA UDANGANYIFU


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Desemba 1, 2022 limetangaza matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2022 ambapo limetangaza kufuta matokeo yote ya Watahiniwa 2194 sawa na asilimia 0.16 ya Watahiniwa 1,350,881 waliofanya mtihani ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022.

Akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2022, Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi  amesema pia NECTA imezifungia shule 24 kuwa vituo vya mitihani ya Taifa baada ya kuthibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Shule hizo ambazo ni sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote vya mitihani nchini, ndani yake zipo shule maarufu ikiwemo ya Musabe ya jijini Mwanza na St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam na shule ya Rweikiza ya mkoani Kagera.


Shule hizo ni Kadama shule ya msingi iliyopo Chato- Geita, Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro shule ya msingi (Arusha) Sahare (Tanga), Ukerewe (Mwanza), Peaceland (Mwanza), Karume (Kagera), Al-hikma (Dar es Salaam), Kazoba (Kagera), Mugini (Mwanza), Busara (Mwanza), Jamia (kagera), Winners (Mwanza), Musabe (Mwanza), Elisabene (Songwe), High Challenge (Arusha), Tumaini (Mwanza), Olele (Mwanza), Mustlead (Pwani).


Pia zipo shule za Moregas (Mara), Leaders (Mara), Kivulini (Mwanza) na St Severine (Kagera).

Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulihusisha watahiniwa zaidi ya 1.38 milioni nchi nzima.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post