MWENYEKITI WA JWT KAGERA NICHOLAUS JOVIN BASIMAKI ATAKA SERIKALI KUFANYA KANZI DATA KWA WAFANYABISHARA WOTE

Mwenyekiti Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Bw. Nicholaus Jovin Basimaki akizungumza katika studio za Radio Vision

***

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Kagera Bw. Nicholaus Jovin Basimaki ameitaka Serikali kufanya kanzi data kwa wafanyabiashara wote ili kusaidia katika ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza na Vision Fm Radio mapema leo Novemba 26,2022 amesema kuwa kanzi data itakapokuwepo itasaidia kupanga vizuri viwango vya tozo na kukusanya tozo bila usumbufu.

"Tunapokuwa na kanzi data itasaidia kujua kama mfanyabiashara huyu amelipa na mwingine hajalipa na siyo hayo mambo ya kufungiana maduka maana unapofunga biashara inakuwa ni kupoteza mapato ya Serikali", amesema Bw. Basimaki.

Ameongeza kuwa biashara inaanzishwa kwa maana ya kuzaliwa, kukua na kufa, hivyo ufanyike utaratibu wa bidhaa zote kuwa na kodi palepale inapoanzia kiwandani ili kuondoa migogoro ya kimaslahi ya kukwepa Kodi.

"Bidhaa inapotoka kiwandani iwe na kodi yake moja kwa moja kwa mfano mfumo uliotumika kwenye ununuzi wa magari imeondoa kero, mtu anaagiza gari anajua Kodi yake ni shilingi ngapi", amesema Bw. Basimaki.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post