BARAZA HURU LA USULUHISHI WA MALALAMIKO YA WANANCHI VIJIJI VINAVYOZUNGUKA MGODI WA MWADUI LAZINDULIWA


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akikata utepe wakati akizindua Taratibu za Baraza la Huru la Usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui kuhusu madhira mbalimbali waliyopata wananchi kwenye mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy kulia ni Simon Mutinda kutoka Kampuni ya Pricewaterhouse Coopers (PWC).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui (Williamson Diamonds Limited) kwa njia ya maridhiano kuhusu madhira ,mbalimbali waliyopata wananchi kwenye mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu limezinduliwa rasmi mkoani Shinyanga.

Uzinduzi wa Baraza la Malalamiko ya Wananchi pamoja na Utaratibu wake katika Mgodi wa Mwadui umezinduliwa leo Jumanne Novemba 29,2022 na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkude amesema matarajio kupitia baraza hilo ni kuona kutenda haki kwa wananchi waliopata madhara kupitia mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu.


“Tunahitaji haki itendeke lakini pia kwa kuzingatia mambo yote tuliyoelezekana ngazi mbalimbali, tuoneshe uhalisia wa haki hizo zinazotolewa na kuwe na tija kwa walengwa wenyewe”,amesema Mkude.


Amesema mara baada ya uzinduzi huo Baraza hilo litaanza kusikiliza malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa Mwadui.


“Utaratibu wa kuunda Baraza Huru la Usuluhishi wa malalamiko ya wananchi ulivyoandaliwa vizuri ukisimamiwa na kufadhiliwa na Petra Diamonds Ltd. Utaratibu wote uliotumika mpaka kufikia leo umekuwa wa wazi na tumekuwa tukieleweshwa ngazi moja hadi nyingine kwa kushirikisha taasisi mbalimbali kuhusu baraza hili la malalamiko na namna likatavyokwenda kufanya kazi”, ameongeza Mkude.

“Lakini nitumie nafasi hii kupongeza imeonekana kwamba Baraza hili likianza kazi kwa ujumla malalamiko yaliyosajiliwa na wananchi yapo 5575 na wameongeza muda wa kuyasikiliza badala ya miaka mitatu imeenda zaidi, hili ni jambo jema, jambo la kiutu ambalo litasaidia kuangalia kwa undani zaidi haki za watu ambazo wamewasilisha malalamiko yao”,ameeleza.


Mkuu huyo wa wilaya amesema serikali itaendelea kushirikiana Baraza hilo wakati wote na pale ambapo panatokea tatizo au viashiria vya shida au tatizo basi jopo zima lisisite kuwasiliana na uongozi ngazi ya mkoa na wilaya ili kutatua mapema matatizo yanayoweza kujitokeza kabla ya kuleta athari kubwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy amesema wana imani Baraza la Huru la Usuluhishi wa malalamiko ya wananchi litafanya kazi kwa weledi mkubwa ili haki iweze kupatikana.

“Petra Diamonds Ltd tukiwa ni wamiliki wa Mgodi wa Mwadui tunatambua changamoto zilizokuwepo, tulifanya mabadiliko mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kukidhi matakwa ya sheria za nchi na kimataifa”,amesema Duffy.

Mwenyekiti wa Jopo Huru la Usuluhishi wa Malalamiko ya Wananchi wanaozunguka mgodi wa Mwadui, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema tangu mwaka 2009 hadi 2021 jumla ya malalamiko 5575 yamesajiliwa na usikilizwaji wa hatua ya awali unaanza mara moja kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa.

“Kila mwananchi aliyesajili malalamiko yake na atayesajili malalamiko yake atafikiwa na Baraza hili kuhusu la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi”,amesema Dkt. Nshala.


Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo kuzinduliwa kwa Baraza Huru la Usuluhusihi wa malalamiko ya wananchi yanayotokana nan a shughuli za uzalishaji wa madini katika mgodi wa Mwadui unafungua Ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya wananchi na mgodi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. William Jijimya ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu kuruhusu kuundwa kwa Baraza hilo huku akilitaka Jopo Huru la Usuluhishi wa Malalamiko ya Wananchi kwenda kufanya kazi kwa weledi na kutenda haki.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akizindua Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui kuhusu madhira mbalimbali waliyopata wananchi kwenye mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema leo Jumanne Novemba 29,2022 Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akizindua Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui kuhusu madhira mbalimbali waliyopata wananchi kwenye mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui kuhusu madhira mbalimbali waliyopata wananchi kwenye mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui kuhusu madhira mbalimbali waliyopata wananchi kwenye mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Jopo Huru la Usuluhishi wa Malalamiko ya wananchi wanaozunguka mgodi wa Mwadui, Dkt. Rugemeleza Nshala akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui.

Mwenyekiti wa Jopo Huru la Usuluhishi wa Malalamiko ya wananchi wanaozunguka mgodi wa Mwadui,Dkt. Rugemeleza Nshala akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui.
Simon Mutinda kutoka Kampuni ya Pricewaterhouse Coopers (PWC) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui ambapo amesema jopo la usuluhishi litaenda kufanya kazi kwa weledi ili jamii ipate suluhisho la malalamiko yao kwa ajili ya kuleta maendeleo katika taifa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. William Jijimya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia) akikata utepe kuzindua Baraza huru la kushughulikia malalamiko ya wananchi ambao wanazunguka Mgodi wa Almasi Mwadui, (kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Petra Diamond Limited Richard Duffy
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude  akikata utepe wakati akizindua Taratibu za Baraza la Huru la Usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji 12 vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui kuhusu madhira mbalimbali waliyopata wananchi kwenye mgodi wa Mwadui uliopo wilayani Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akionesha Vitendea kazi vya Baraza Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi katika mgodi wa Mwadui
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akimkabidhi Vitendea kazi vya baraza huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi katika mgodi wa Mwadui Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese Vitendea kazi vya baraza huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi katika mgodi wa Mwadui
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniphace Butondo, Vitendea kazi vya baraza huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi katika mgodi wa Mwadui
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. William Jijimya  Vitendea kazi vya baraza huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi katika mgodi wa Mwadui
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited, inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Richard Duffy (kushoto) wakikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Jopo Huru la Usuluhishi wa Malalamiko ya wananchi wanaozunguka mgodi wa Mwadui, Dkt. Rugemeleza Nshala na Simon Mutinda kutoka Kampuni ya Pricewaterhouse Coopers (PWC).

Zoezi la makabidhiano ya Vitendea kazi vya baraza huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi katika mgodi wa Mwadui likiendelea
Zoezi la makabidhiano ya Vitendea kazi vya baraza huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi katika mgodi wa Mwadui likiendelea
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo Kishapu

Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo Kishapu
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo Kishapu
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited wakipiga picha na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Petra Diamonds Limited wakipiga picha na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Baraza la Huru la usuluhishi wa malalamiko ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo Kishapu.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post