POLISI WACHARUKA MREMBO KUANIKA MAKALIO UWANJANI


Polisi nchini Italia wanaripotiwa kuanzisha uchunguzi dhidi ya mwanamitindo aliyeonyesha makalio yake wakati wa michezo uwanjani.

Coyotee Cuttee ambaye ni mtayarishaji wa maudhui ya watu wazima, huendesha akaunti kwa jina Only Fans, anasemekana kuwa shabiki mkubwa wa mechi za Serie B, ambapo aliishia kuanikia mashabiki makalio yake uwanjani.

Only Fans ni mtandao ambao hutumika kwa maudhui ya watu wazima pekee na hutumika hususan kwa wafanyakazi wa kuzalisha video za ngono. The Sun linaripoti kuwa Coyotee Cuttee ni shabiki sugu wa klabu ya Serie B, Bari.

Ukurasa wake wa Instagram, ambao ni wa faragha, una picha zake akiwa kwenye uwanja wa San Nicola, huku makalio yake yakionekana.

The Sun linaongeza zaidi kwamba hukana kuwa sio mtayarishaji wa maudhui ya filamu za watu wazima. 

Haijulikani ni mashtaka gani anayoweza kushtakiwa nayo, lakini kuanika uchi hadharani ni marufuku katika mataifa kadhaa ulimwenguni na iwapo mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22, atapatikana na hatia atafungwa jela ama kupigwa faini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post