MWANAFUNZI AJIFUNGUA WATOTO WATANO



Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu amegonga vichwa vya habari baada ya kujifungua watoto watano.

Mwanafunzi huyo alibarikiwa na bahati hiyo ya kutokea kwa nadra mno huku mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu ukiendelea nchini mwao.

Kulingana na taarifa zilizochapishwa na Staelitte huko Nigeria, mwanafunzi huyo kwa jina Oluomachi Linda Nwojo, aliwakaribisha watoto hao mwendo wa saa 9:02 usiku wa Jumatatu, Oktoba 3.


Binti huyo wa miaka 24 alipata mapacha 5 wakiwemo wa kiume wawili na mabinti watatu, na ndio mara ya kwanza kutokea katika kituo hicho cha hospitali, kulingana na ripoti hiyo.


Huku kampeni zikiwa zimepamba moto nchini Nigeria, vyanzo viliripoti kuwa mrengo fulani wa kisiasa uliingilia kati na kulipa bili ya hospitali ili mama huyo kuruhusiwa kutoka na watoto wake wote watano waliozaliwa salama salimini.


Hata kama kulikuwepo na mkanganyiko katika taarifa, baadhi ya watu walikuwa wanasema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ameoleka haswa baada ya jamaa mmoja kuibuka kwenye mitandao na kupakia kuwa ni mkewe aliyezaa watoto hao mapacha 5.


Wengine walisema kuwa binti huyo alizungumza mwenyewe na kukanusha madai ya kuolewa, ambapo alisema kuwa yeye bado yupo singo ila akadinda kufichua mhusika wa mimba hiyo ya ajabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments