SUNGUSUNGU WASIMIKA VIONGOZI WAPYA, DC MBONEKO AWATAKA KUKOMESHA VIBAKA MITAANIMkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JESHI la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini limewasimika viongozi wapya wa Jeshi hilo, huku Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka kukomesha vibaka mitaani.


Usimikaji wa viongozi hao wapya Sita wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini umefanyika leo Oktoba 13, 2022 katika bwalo la Jeshi la Polisi Manispaa ya Shinyanga.

Mboneko akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, amelitaka Jeshi hilo la Jadi kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama katika mitaa yote, ikiwamo na kudhibiti wimbi la vibaka Mitaani ambao wamekuwa wakipora vitu mbalimbali zikiwamo Simu na Pochi za akina mama.

“Naagiza Jeshi hili la Jadi Sungusungu liwepo kwenye kila Kata Manispaa ya Shinyanga, ili kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama, sababu Polisi hawatoshi kufanya kazi peke yao, tunataka uhalifu uishe mitaani kusiwepo na vibaka wala watu kukatwa mapanga hovyo kama ilivyotokea huko Kolandoto,”amesema Mboneko.

Katika hatua nyingine, amelitaka Jeshi hilo la Jadi kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kwenye maeneo yao, ili kusiwepo wizi wa aina yoyote ile wa vifaa, pamoja na kuacha kuwapa adhabu viongozi wa Serikali bali wao wana mamlaka ambazo zinawashughulikia.

Pia amewataka Sungusungu kuzuia ndoa za utotoni kwa wanafunzi ambao wamehitimu elimu ya darasa la saba ili matokeo yakitoka wote wakutwe wapo na salama na kuendelea na masomo yao kidato cha kwanza.

Naye Afisa Taarafa wa Shinyanga Mjini Charles Maugila, amesema sasa hivi vibaka wamezidi mitaani, na kuliomba Jeshi hilo la Jadi Sungusungu liwashughulikie.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mpya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga Mjini Paulo Madale, ameahidi Jeshi hilo litafanya kazi zake kwa weledi kukomesha uhalifu mitaani, pamoja na fedha ambazo watakuwa wakitoza faini zitakuwa zikipelekwa kwenye miradi ya maendeleo.

Viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini ambao wamesimikwa ni Paul Madale ambaye ni Mwenyekiti, Makamu wake Juma Mipawa, Katibu Mkuu ni Ngaja Ngasa, Msaidizi wake Lucas Shija, Kamanda Mkuu ni Thomas Mwita, Msaidizi wake Rashidi Ngoeji.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye kikao cha usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini.

Afisa Tarafa wa Shinyanga mjini Charles Maugila akizungumza kwenye kikao cha usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini.

Makamu Mwenyekiti wa Jeshi la Jadi Sungusungu Manispaa ya Shinyanga Idd Pyalimu, akizungumza kwenye kikao cha usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini.
 
 Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jadi Sungusungu Manispaa ya Shinyanga John Kadama, akizungumza kwenye usimikaji huo wa viongozi wapya wa Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini.

Mwenyekiti mpya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini Paul Madale akizungumza mara baada ya kumaliza kusimikwa.

Viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini wakisimikwa rasmi kulitumikia Jeshi hilo.

Viongozi wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) kutoka Kata Mbalimbali Tarafa ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye kikao cha usimikwaji viongozi wapya wa Jeshi hilo tarafa ya Shinyanga mjini.

Zoezi la usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.

Zoezi la usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.

Zoezi la usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.

Zoezi la usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.

Zoezi la usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.
Zoezi la usimikaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.

Viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini wakisimikwa rasmi kulitumikia Jeshi hilo.
 
 
 
 
 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post