SHUWASA WALIANGUKIA JESHI LA JADI SUNGUSUNGU UHARIBIFU MIUNDOMBINU YA MAJI



Afisa Mahusiano na Umma kutoka (SHUWASA) Nsianel Gerald akizungumza kwenye zoezi la usimikwaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), wameliomba Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini, kukomesha vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya maji.


Afisa Mahusiano na Umma kutoka (SHUWASA) Nsianel Gerald amebainisha hayo leo Oktoba 13, 2022 kwenye zoezi la usimikwaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini katika ukumbi wa bwalo la Jeshi la Polisi Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati akitoa salamu za Mamlaka hiyo ya Maji (SHUWASA) amesema sasa hivi kumekuwapo na tatizo la watu kuharibu miundombinu ya maji, na kusababisha wananchi kukosa huduma ya maji, huku wao wakiingia hasara ya ununuzi wa vifaa vya matengenezo, fedha ambazo zingesaidia kuboresha huduma zaidi na kupanua wigo wa mtandao wa maji.

“Tunaliomba Jeshi la Jadi Sungusungu litusaidie kuzuia uharibifu wa miundombinu ya maji, sasa hivi limekuwa tatizo kubwa na kusababisha wananchi kukosa huduma ya maji,”amesema Gerald.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ambaye alikuwa mgeni Rasmi kwenye zoezi hilo, amelitaka Jeshi la Jadi Sungusungu liwepo kila Kata, pamoja na kudhibiti matukio ya uhalifu ili wananchi wabaki kuwa salama pamoja na mali zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mpya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga Mjini Paulo Madale, ameahidi Jeshi hilo litafanya kazi zake kwa weledi kukomesha matukio ya uhalifu mitaani.

Viongozi wapya wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga mjini ambao wamesimikwa leo ni Paul Madale ambaye ni Mwenyekiti, Makamu wake Juma Mipawa, Katibu Mkuu ni Ngaja Ngasa, Msaidizi wake Lucas Shija, Kamanda Mkuu ni Thomas Mwita, Msaidizi wake Rashidi Ngoeji.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye zoezi la usimikwaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini.

Afisa Mahusiano na Umma kutoka (SHUWASA) Nsianel Gerald akizungumza kwenye zoezi la usimikwaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini.

Mwenyekiti mpya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini Paul Madale akizungumza mara baada ya kumaliza kusimikwa.
Baadhi ya watumishiwa SHUWASA wakiwa kwenye kikao cha usimikwaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini.
Zoezi la usmikwaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.
Zoezi la usmikwaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.
Zoezi la usmikwaji viongozi wapya wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini likiendelea.
Viongozi wapya sita wa Jeshi la Jadi (Sungusungu) Tarafa ya Shinyanga mjini wakisimikwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments