MKURUGENZI TPDC AKAGUA UJENZI KIWANDA CHA KUFUNIKA MABOMBA SOJO - NZEGA MRADI BOMBA LA MAFUTA ..."MNUFAIKA AFURAHIA NYUMBA ZA KISASA"

Muonekano wa  moja ya nyumba za mnufaika wa mradi
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kufunika mabomba katika kijiji cha Sojo, William Kajagi (katikati) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kushoto) kuhusu ujenzi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga na kujionea shughuli mbalimbali za ujenzi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Dk. Mataragio amefanya ziara hiyo leo Alhamisi Septemba 15,2022 katika kambi ya kijiji cha Sojo kata ya Igusule pamoja na kumtembelea mmoja wa wanufaika wa mradi huo, Kazimila Patrick Mshandete ambaye alikubali kutoa eneo lake kwa ajili ya kupisha mradi huo ambapo Serikali imemlipa fidia na kumjengea nyumba za kisasa na kuendelea kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo chakula kila mwezi.

Akizungumza katika Kambi hiyo ya Sojo, Dk. Mataragio amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Mradi huo ambapo kazi za awali za ujenzi wa Kiwanda cha Kufunika Mabomba zimefikia 60% huku akieleza kufurahishwa zaidi kuona fursa mbalimbali za ajira zikitolewa kwa wananchi wazawa wanaozunguka mradi huo.

“Nimefurahi kuona kazi ya ujenzi wa mradi inaendelea vizuri na wazawa zaidi ya 180 wamepata ajira katika kazi hizi za awali. Serikali ilisaini Mkataba wa Msingi wa Mradi (Host Government Agreement (HGA) kati yake na Mwekezaji, Kampuni ya EACOP ambapo, kupitia Mkataba huo umeainisha baadhi ya huduma na bidhaa zitakazotolewa na Watanzania pekee ikiwemo huduma za usafirishaji, ulinzi, chakula na vinywaji, huduma za malazi na usambazaji wa mafuta kwa ajili ya magari na mitambo nafurahi kuona wazawa wanaendelea kufanya kazi katika kambi hii”,amesema Dk. Mataragio.

“Hizi ni kazi za awali tu, bado kuna fursa nyingi za ajira hadi mradi utakapokamilika. Nimefurahi pia kuona Makampuni ikiwemo Vodacom kujenga mnara wa mawasiliano hapa, naomba wadau na makampuni mbalimbali yalete huduma za kijamii hapa. Watanzania changamkieni fursa zitakazotokana na ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania ili kujiongezea kipato na utaalamu kwani sehemu kubwa ya bomba linapita nchini Tanzania”,amesema Dk. Mataragio.

“Mradi huu ni wa muhimu kwa nchi yetu kwani asilimia, 80 ya bomba hili lipo upande wa Tanzania hivyo nawaomba watanzania wachangamkie fursa zitakazotokana na utekelezaji wa mradi huu” amesisitiza Dk. Mataragio.

Akiwa katika makazi mapya ya mnufaika wa mradi huo, Kazimila Patrick Mshandete mkazi wa kijiji cha Sojo ambaye ni miongoni mwa wakazi zaidi 300 waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, Dk. Mataragio amesema imelipa fidia kwa wananchi na wengine kuwajengea nyumba za kisasa huku akibainisha kuwa taratibu zote zikiwemo za kimataifa zimezingatiwa.

“Tumefuata taratibu zote, tumewalipa fidia na kuwajengea nyumba za kisasa hivyo hakuna ukiukwaji wowote wa haki za binadamu. Tunatekeleza Mradi huu kwa uwazi mkubwa na tunazingatia haki za binadamu, hakuna haki inayokiukwa”,ameeleza Dk. Mataragio.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kufunika mabomba katika kijiji cha Sojo, William Kajagi amesema wanaendelea na ujenzi wa msingi wa kiwanda cha kufunika mabomba kwa kutengeneza mfumo wa kuzuia joto lisipotee na hadi kufikia Mwezi Januari 2023 wanatarajia kuanza uzalishaji.

Naye mnufaika wa mradi huo, Kazimila Patrick Mshandete amesema tangu mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta uanze kumekuwa na ushirikishwaji wa wanakijiji hatua kwa hatua na kwa uwazi na wananchi wameshalipwa fidia na wale waliotaka kujengewa makazi wameshajengewa nyumba za kisasa na wanapatiwa huduma mbalimbali ikiwemo chakula kila mwezi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (katikati) akizungumza leo Alhamisi Septemba 15,2022 katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kufunika mabomba katika kijiji cha Sojo, William Kajagi (katikati) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kushoto) kuhusu ujenzi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Muonekano maendeleo ya ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kulia) akizungumza wakati akikagua ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kufunika mabomba katika kijiji cha Sojo, William Kajagi (katikati) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kulia) kuhusu ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Mratibu Mradi wa EACOP, Safiel Msovu (katikati) akizungumza wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kulia) akikagua ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kufunika mabomba katika kijiji cha Sojo, William Kajagi (katikati) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kulia) kuhusu ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio  ( wa pili kushoto) akizungumza na Mzee Kazimila Patrick Mshandete (kulia) mkazi wa kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora ambaye ni mnufaika wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga. Mwananchi huyo alikubali kutoa eneo lake la hekari 6 kwa ajili ya kupisha mradi huo ambapo Serikali imemlipa fidia na kumjengea nyumba za kisasa na kuendelea kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo chakula kila mwezi. 
Mzee Kazimila Patrick Mshandete (kulia) mkazi wa kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora ambaye ni mnufaika wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga akiishukuru serikali kumjengea nyumba za kisasa na kupongeza jinsi mradi huo unavyotekelezwa kwa uwazi na kuzingatia haki za binadamu.
Muonekano wa  moja ya nyumba za mnufaika wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, Mzee Kazimila Patrick Mshandete mkazi wa kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora aliyejengewa nyumba za kisasa baada ya kukubali kupisha eneo lake kwa ajili ya mradi huo wa mafuta.

Muonekano wa  nyumba za mnufaika wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, Mzee Kazimila Patrick Mshandete mkazi wa kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora aliyejengewa nyumba za kisasa baada ya kukubali kupisha eneo lake kwa ajili ya mradi huo wa mafuta.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments