WAZIRI DKT MABULA AIPA WIKI MBILI HALMASHAURI YA SERENGETI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza na uongozi wa wilaya ya Serengeti na watendaji wa sekta ya ardhi tarehe 12 Julai 2022Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti (aliyevaa Kaunda) Ayoub Mwita akimuonesha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi eneo la kijiji cha Nyichoka katika ramani ya Sereneti wakati wa ziara ya siku moja katika wilaya hiyo tarehe 12 Julai 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiangalia moja ya hati za kimila alizozikuta katika ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Serengeti wakati wa ziara yake ya siku moja tarehe 12 Julai 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

***************

Na Munir Shemweta, SERENGETI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameipa wiki mbili halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara kumpatia taarifa ya hali ya mashamba 36 yaliyopo katika halmashauri hiyo ili yale mashamba yasiyoendelezwa yaweze kubatilishwa umiliki wake.

Hatua hiyo inafuatia kuelezwa kupitia taarifa ya sekta ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Serengeti kuwa wilaya hiyo ina mashamba yaliyopimwa 36 kulingana na taarifa iliyopatikana kutoka wizarani kutokana na kutokuwepo kumbukumbu za kutosha mashamba hayo katika wilaya hiyo.

Taarifa hiyo iliyosomwa na nAfisa Ardhi Mteule wa Halmasahauri hiyo ya Serengeti Orwaka Nyamsusa ilieleza kuwa, mashamba hayo yalipimwa vijijini bila kufuata taratibu za uhaulishaji na ilipotakiwa yamililishwe kwa kupewa hati za kawaida ilishindikana.

"Ninawapa Serengeti wiki mbili nijue status ya mashamba hayo na kama ni suala la kuanza kuyabatilisha, mchakato uanzie katika halmashauri ambayo ni mamlaka ya upangaji ili tuitangaze fursa kwa wawekezaji kama Serengeti tunayo mashamba 36 na kati ya hayo ni matano tu yenye umiliki halali’’. Alisema Dkt Mabula

Akizungumza na uongozi wa wilaya ya serengeti na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo tarehe 12 Juala 2022 wilayani humo, Dkt Mabula alisema haingii akilini mashamba pamoja na ardhi kuwa katika halmashauri hiyo lakini halmashauri husika haina kumbukumbu iwapo imeyapima mashamba hayo na badala yake inaenda kutafuta kumbukumbu wizarani.

Alibainisha kuwa, kama utaratibu wa kuisimamia sekta ya ardhi kwa halmashauri ya Serengeti utakuwa ni wa aina hiyo basi halmashauri hiyo haiwezi kufika popote katika masuala ya ardhi na itaendelea kuwa na changamato.

" Halmashauri ni mamlaka za upangaji kwa mujibu wa sheria namba 8 ya mipango miji ya 2007, ni mamlaka za upangaji zinazotakiwa kupanga miji yao wanataka iwe ya namna gani wizara kazi yake ni kusimamia na kuangalia kama shughuli za ardhi zinaenda kwa utaratibu au shetia zinafuatwa.

Alisema, halmashauri nyingi hazifuati takwa la sheria huku zikifahamu ni mamlaka za upangaji na kueleza kuwa halmashauri zote zinatakiwa kutekeleza takwa hilo na zisipotekekeza migogoro yq ardhi haiwezi kuisha.

Katika taarifa yake, halmashauri ya wilaya ya serengeti ilieleza kuwa wilaya hiyo ina jumla ya vijjji 78 ambapo kato ya hivyo vijjji 61 vimepimwa huku vijiji 10 kati ya hivyo vikitakiwa kufanyiea marejeo kutokana na makosa katika ramani za upimaji.

Aidha, jumla ya vijiji 29 kati ya 78 vina mpango wa matumizj bora ya ardhi ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/ 2023 halmashauri hiyo imetenga kiaai cha shilingi 15,000,000 kwa ajili ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji 3

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments