MMOJA WA PACHA WALIOTENGANISHWA AFARIKI DUNIA


Pacha waliotenganishwa

Mmoja wa pacha aitwaye Neema waliotenganishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili amefariki dunia Julai 10, 2022. Aidha mwenzake aitwaye Rehema anaendelea vizuri.

Taarifa iliyotolewa na Hospitali hiyo leo Julai 12, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel Aligaesha, imeeleza kuwa hali ya Neema ilibadilika ghafla akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

"Tuendelee kumuombea Rehema ambaye bado yupo ICU ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema. Bwana alitoa na Bwana ametoa, jina lake lihimidiwe sana," amesema Aligaesha

Mapacha hao Neema na Rehema, walifanyiwa upasuaji Julai Mosi mwaka huu, ambapo kwa mujibu wa hospitali hiyo upasuaji huo ulifanyika na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post