DC MBONEKO AIPONGEZA SHUWASA KUTEKELEZA KIKAMILIFU MIRADI YA MAJI FEDHA ZA UVIKO - 19...."CHENJI IMEBAKI'Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) akimtwisha ndoo ya Maji Ashura Masanja mkazi wa kijiji cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.
 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua mradi wa Maji katika kijiji cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga utokanao na fedha za UVIKO-19 ambao umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa Miradi ya Maji ya fedha za UVIKO-19, ambayo inatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.


Mboneko amefanya ziara hiyo leo Julai 11,2022 akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama wilaya, pamoja na Menejimenti ya Mamlaka hiyo ya maji (SHUWASA) kwa kukagua miradi ya Maji halmashauri ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa Miradi hiyo ya Maji, Mboneko amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za UVIKO-19 na kutekeleza Miradi ya Maji kwa wananchi, ambayo imewaondolea adha ya matumizi ya Maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu, na kuyafuata umbali mrefu.

Amesema ameamua kufanya ziara hiyo ya kukagua miradi ya maji ya fedha za UVIKO-19, ili kuona utekelezaji wake na kiwango cha thamani ya fedha, na kuonyesha kuridhishwa na ujenzi wa miradi hiyo, ambayo imeanza kutoa huduma ya Maji safi na salama kwa wananchi.

"Nawapongeza sana SHUWASA kwa kusimamia vizuri fedha hizi za UVIKO-19, nimeona utekelezaji wa miradi hii ya maji ipo vizuri na inatoa huduma kwa wananchi, na fedha mmezitumia vizuri na chenji imebaki,"
amesema Mboneko.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi waitunze miundombinu hiyo ya Maji, pamoja na kuunganisha maji majumbani mwao, ili wapate huduma karibu na kuacha kutembea umbali mrefu na kupoteza muda wa kufanya shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, amesema walipokea fedha za (UVIKO-19) Sh. milioni 469 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, na wametumia Sh.milioni 406, huku akibainisha kuwa wameshaleta Mita za Maji 2,400 na kuwaomba wananchi watume maombi ya kuunganishiwa maji.

Nao baadhi ya wananchi waliopata huduma hiyo ya Majisafi na Salama, wameipongeza Serikali kwa kuwapatia maji, ambayo yamewasaidia kuondokana na changamoto mbalimbali zitokanazo na ukosefu wa Majisafi.

Miradi ya Maji ambayo ametembelea Mkuu huyo wa Wilaya ni Kijiji cha Magwata, Bugwandege, Bugimbagu, Didia, Iselamagazi, pamoja na ujenzi wa Tenki la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Tinde hadi Shelui.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi ya Maji ambayo inatekelezwa na fedha za UVIKO-19 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassani.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi ya Maji ambayo inatekelezwa na fedha za UVIKO-19 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga na kuwataka waitunze miradi ya maji, pamoja na kuunganisha maji majumbani mwao. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bugimbagu Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga na kuwataka waitunze miradi ya maji, pamoja na kuunganisha maji majumbani mwao.

Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ya ukaguzi wa miradi ya maji itokanayo na fedha za UVIKO-19 ambayo wanaitekeleza na yote imekamilika na kutoa huduma kwa wananchi.

Ashura Masanja mkazi wa kijiji cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga akishukuru kupata huduma ya Majisafi na Salama.

Mwananchi Samson Paulo kutoka kijiji cha Bubale wilayani Shinyanga, ambaye amefuata huduma ya Maji safi na Salama katika kijiji jirani cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga akishukuru kutekelezwa mradi huo wa maji.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua mradi wa Maji katika kijiji cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga utokanao na fedha za UVIKO-19 ambao umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua mradi wa Maji katika kijiji cha Bugwandege Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga utokanao na fedha za UVIKO-19 ambao umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua mradi wa Maji katika kijiji cha Bugimbagu Kata ya Mwawaza Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga utokanao na fedha za UVIKO-19 ambao umetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

Ukaguzi wa miradi ya maji ukiendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) akimtwisha ndoo ya Maji Ashura Masanja mkazi wa kijiji cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia) akimtwisha ndoo ya Maji Samsoni Paulo mkazi wa kijiji cha Bubale wilayani Shinyanga.
Ukaguzi miradi ya maji ya fedha za UVIKO-19 ukiendelea.

Ukaguzi miradi ya maji ya fedha za UVIKO-19 ukiendelea.

Ukaguzi miradi ya maji ya fedha za UVIKO-19 ukiendelea.

Ukaguzi miradi ya maji ya fedha za UVIKO-19 ukiendelea.

Ukaguzi miradi ya maji ya fedha za UVIKO-19 ukiendelea.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipanda ngazi kukagua ujenzi wa Tenki la Maji katika Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kutoka Tinde hadi Shelui.

Ukaguzi ujenzi wa Tenki la Maji ukiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akishuka mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa Tenki la Maji katika Mradi wa Maji Ziwa Victoria kutoka Tinde hadi Shelui.

Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maji ya fedha za UVIKO-19 ukiendelea.

Ukaguzi miradi ya maji ya fedha za UVIKO-19 ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post