AJALI YAUA WATU NANE, WATANO FAMILIA MOJANa Mbuke Shilagi Kagera.

Watu nane wamefariki dunia kwa ajali ya magari mawili yaliyo gongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu nane,huku watano wakiwa ni familia moja huko Biharamulo Mkoani Kagera.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 13, 2022 ofisini kwake, Kamanda wa jeshi la polisi ACP William Mwampaghale amesema kuwa ajali hiyo mbaya imetokea katika maeneo ya Busiri katika barabara kuu ya kutoka Lusahunga kuelekea Nyakahura Wilaya ya Biharamulo mnamo tarehe 11 Julai 2022.

Na kwamba gari lenye namba za usajili RAF 129W likiwa na Treila lenye namba RL 4367 aina ya Mercedes-Benz lililokuwa likiendeshwa na Vicent Gakuba Mnyarwanda mwenye miaka 52, gari hilo lilikuwa likitokea Rwanda na kuelekea Dar es saalam ambapo liligongana uso kwa uso na gari namba T. 626 DRX aina ya Toyota Succeed lililokuwa likitokea Nyamalagala na kuelekea Benako lililokuwa likiendeshwa na Nyawenda Bihela mwenye miaka 35.

ACP Mwampaghale amesema kuwa  ajali hiyo imesababisha vifo vya watu nane ambao ni dereva na mmiliki wa gari ya Toyota Succeed pamoja na abiria wake saba waliokuwemo kwenye gari hilo, huku watano miongoni mwao wakiwa ni wa familia moja (Mama na watoto wanne).

Na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari namba RAF 129W Mercedes Benz, uliotokana na kuhama upande wa kushoto wa barabara na kuendesha upande wa kulia uliopelekea kugongana uso kwa uso.

Dreva huyo alijaribu kutoroka mara baada ya ajali lakini jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata katika kizuizi cha Kahaza Rusumo akiwa ndani ya lori linaloelekea Rwanda, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Jeshi la polisi linatoa onyo kwa madreva wazembe wasiofata sheria za usalama barabarani kubadilika mara moja kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments