MGEJA AKUTANA NA ASKOFU NKWABI..AWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KULIOMBEA TAIFA


Askofu wa kanisa la T.C.G.I Simon Nkwabi amefanya ziara ya kumtembelea Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mzee Hamis Mgeja ofisini kwake Kahama Motel na kufanya nae mazungumzo kuhusu mustakabali wa nchi, kisiasa, kiuchumi na kijamii.


Mzee Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa  taasisi inayojishughulisha na masuala ya haki, Demokrasia na utawala bora nchini ametumia nafasi hiyo kumpongeza Askofu Mkuu Simon Nkwabi kwa niaba ya viongozi wa dini nchini kwa kazi kubwa ya kuendelea kuliombea taifa na viongozi wake akiwemo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.


Askofu Simon Nkwabi amesema wao kama viongozi wa dini nchini wataendelea kuliombea Taifa usiku na mchana pamoja na kumuombea Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliongoza taifa kwa amani, upendo na usawa.
Pia askofu Mkuu Saimon Nkwabi amefanya maombi mafupi ya kumtakia Kheri mzee Khamis Mgeja katika maisha yake ya kila siku na kumuomba Mungu amzidishie hekima na busara huku akimpongeza kwa kuwa mpenda haki na mkweli na mpenda kushirikiana na jamii bila ubaguzi wa dini, ukabila na ukanda.


Katika shughuli hiyo ya maombi yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa manispaa wa Kahama na halmashauri ya Msalala na Ushetu wakiwemo na baadhi ya wazee wa Manispaa ya Kahama, akiwemo na katibu Mkuu wa Chama Cha Kutetea haki za wanaume nchini Antony Solo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments