RAIS SAMIA AWAHIMIZA MAKATIBU MAHSUSI KUTUNZA SIRI ZA SERIKALI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Zawadi Maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) Bi. Zuhura Songambele Maganga kabla ya kufungua Mkutano huo Mkuu wa Kitaaluma kwa Makatibu hao Mahsusi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

Baadhi ya Viongozi na Makatibu Mahsusi kutoka Ofisi mbalimbali za Serikali Tanzania Bara na Zanzibar wakicheza katika Sherehe ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

Makatibu Mahsusi kutoka Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakiimba na kushangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

Makatibu Mahsusi kutoka Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Makatibu Mahsusi wa Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) kwa ajili ya Makatibu hao nchini katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wasanii wa Chuo cha Utumishi wa Umma mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na baadhi ya Mawaziri, viongozi wa TAPSEA pamoja na Wasanii wa Chuo cha Utumishi wa Umma katika picha ya pamoja na Kwaya ya Utumishi wa Umma mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

***************************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Makatibu Mahsusi, Watunza Kumbukumbu pamoja na maafisa Utumishi kutunza siri za Serikali.

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akifungua Mkutano wa Tisa (09) wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).

Aidha, Rais Samia amesema suala la utunzaji wa siri za Serikali linasaidia kuepuka madhara yanayoweza kuwapata watu binafsi, Taasisi, Serikali na usalama wa Taifa letu.

Rais Samia pia amesema weledi, uaminifu, uadilifu na uzalendo ndiyo njia pekee itakayowafanya Makatibu Mahsusi kuaminiwa, kutegemewa na kuwawezesha kusonga mbele katika majukumu yao.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameridhia Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora kuwa maalum kwa ajili ya mafunzo ya uhazili kwa ngazi zote ili kuzalisha Makatibu Mahsusi ambao watakwenda kutumika katika Taasisi za Serikali.

Halikadhalika, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundo mbalimbali ya kada za kiutumishi, na maslahi ya watumishi wa umma kwa ujumla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments