" MWANAMKE MWINGINE AUAWA JIJINI MWANZA...ADAIWA KUCHOMWA KISU KISHA KUNYONGWA NA MZAZI MWENZIE

MWANAMKE MWINGINE AUAWA JIJINI MWANZA...ADAIWA KUCHOMWA KISU KISHA KUNYONGWA NA MZAZI MWENZIE

Ashura aliyenyongwa
**
Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Aisha mkazi wa Buswelu mkoani Mwanza, amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake kwa kudaiwa kuchomwa kisu na kunyongwa shingoni na mzazi mwenzake ambaye hivi karibuni walikuwa na migogoro ya mapenzi.

Tukio hilo limetokea nyumbani kwa mwanamke huyo mtaa wa Nyamadoke, Kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela, ambapo mfanyakazi wa Aisha ajulikanaye kama Christina Paulo, amesema dada yake huyo amekuwa akigombana mara kwa mara na mzazi mwenzake ambaye walikuwa wametengana.

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Aisha mkazi wa Buswelu mkoani Mwanza, amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake kwa kudaiwa kuchomwa kisu na kunyongwa shingoni na mzazi mwenzake ambaye hivi karibuni walikuwa na migogoro ya mapenzi.

Chanzo - EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments