Post Top Ad
Sunday, May 29, 2022
COASTAL UNION YAINYOOSHA AZAM FC...SASA KUKUTANA NA YANGA SC FAINALI ASFC
Na Emmanuel Mbatilo
KLABU ya Coastal Union imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali kombe la Azam Sprots Federation Cup mara baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 6-5 dhidi ya timu ya Azam Fc katika mchezo uliochezwa leo katika Dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha
Mchezo huo ambao ulimalizika kwa dakika 90 kwa timu zote bila kupata bao na kufanya kwenda dakika 30 za nyongeza nako timu hazikupata bao nakwenda hatua ya mikwaju ya penati.
Katika mchezo huo ambao ulichezwa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha uliibua hisia kubwa za mashabiki kwani timu zote mbili zilionesha kandanda safi japokuwa walitengeneza nafasi nyingi za wazi bila mafanikio.
Sasa Coastal Union wanatinga hatua ya fainali ambapo watakutana na Yanga Sc mchezo ambao utapigwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Malunde 1 blog ni blog ya Kiswahili maarufu duniani kwa habari za Matukio, Siasa, Magazeti, Nyimbo za asili na habari za kusisimua.
fainali itakuwa ln tarehe
ReplyDelete