MAKAMU WA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR AFUNGUA MAONESHO YA MAKISATU - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, May 17, 2022

MAKAMU WA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR AFUNGUA MAONESHO YA MAKISATU


Na Imma Msumba -  Dodoma
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Mei 16,2022 amemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika Hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Taifa ya Ubunifu pamoja na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka huu wa 2022.
 
Akizungumza wakati akifungua maonesho hayo mgeni rasmi Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amewataka watu mbalimbali wenye uwezo wa kuonesha bunifu mbalimbali kuendelea kujitokeza ili serikali ione namna itakavyowaunga mkono.

“Nimeridhika na mambo niliyo ona wakati napitia mabanda ya maonesho. Inaonekana kuna hatua kubwa iliofikiwa katika ubunifu wa bidhaa kwa kutumia teknolojia mbalimbali za kisasa”, alisisitiza


Hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma Tanzania na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Kidini na wa Kimila, Vyama vya Siasa, Wananchi, Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Waandishi wa Habari, Wanafunzi, Vikundi vya Burudani, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na Vijana wabunifu.


Pamoja na kuhutubia hafla hiyo, Mheshimiwa Othman aliyeambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, alipata fursa ya kutembelea Mabanda mbali mbali ya Maonyesho ya Ubunifu na pia kupata maelezo ya Wajasiriambali kutoka Ndani na Nje ya Nchi, yakiwemo Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages