RAIS SAMIA ATEMBELEA BANDA LA STAMICO IKITANGAZA MKAA MBADALA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, May 3, 2022

RAIS SAMIA ATEMBELEA BANDA LA STAMICO IKITANGAZA MKAA MBADALA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse akimwelezea Mhe. Rais Samia kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya. 

Dkt. Mwasse amesema Mkaa huo mbadala ni suluhisho la Nishati Mbadala kwa ajili kupikia ikiwa ni mkakati wa STAMICO katika kutunza mazingira na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi "Tumeshiriki kwenye maadhimisho haya ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani tukiamini kuwa hili ni jukwaa kuu na sahihi la waandishi wa habari ili bidhaa hii iingie sokoni haraka na waandishi wa habari wawe mabalozi wa kuelimisha jamii na kutangaza Nishati hii mbadala' , amesema Dkt. Mwasse.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kushoto) akimwelezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kushoto) akimwelezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

No comments:

Post a Comment

Pages