WIZARA YA AFYA YATANGAZA AJIRA MPYA



Wizara ya Afya nchini Tanzania kupitia kwa Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Abel Makubi imetangaza nafasi za ajira 1650 kwa wataalamu wa kada mbalimbali za afya nchini.


Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa imepata kibali cha kuajiri ambapo wataalamu hao wataajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi ambavyo vipo chini ya uendeshaji wa moja kwa moja wa wizara hiyo.

Miongoni mwa nafasi hizo, zipo za madaktari bingwa (25), madaktari (215), wafamasia(15), maafisa maabara(62), wateknolojia (dawa, maabara, mionzi, macho-155), maafisa uuguzi (140), maafisa uuguzi wasaidizi (467), wauguzi (140), wakemia (2),

Wengine ni madaktari wa afya kinywa na meno (15), tabibu meno (19), watoa tiba kwa vitendo (15), wazoeza viungo kwa vitendo(31), maafisa wazoeza viungo (33), maafisa afya mazingira(40), wasaidizi wa afya (134), wahandisi vifaa tiba (17), wateknolojia vifaa tiba (40) , watunza kumbukumbu wa wfya (10) na madereva (4).
 
Via - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments