WATU 6 WAFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA GARI TANGA


Picha kutoka eneo la tukio

Watu 6 wamefariki Dunia katika ajali ya gari na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la Nyasa Barabara ya kutoka Lushoto kwenda Mombo.

Ajali hiyo imehusisha Fuso yenye namba za usajili T 239 AFD lililokuwa limebeba bidhaa za sokoni kutokea Wilaya ya Lushoto kwenda Handeni.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kwa taarifa za awali watu 4 ndio waliopoteza maisha na baadaye waliongezeka wengine wawili ambao walikuwa majeruhi.

"Waliotutoka mwanzoni walikuwa wanne lakini wameongezeka majeruhi wawili na jumla kufikia 6 ambapo kati yao waliofariki wanaume ni 4 na wanawake ni wawili," amesisitiza Kamanda Jongo.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments