WAHUNI WATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZA MAKARANI WA SENSA... OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAHADHARI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Monday, March 28, 2022

WAHUNI WATANGAZA NAFASI ZA KAZI ZA MAKARANI WA SENSA... OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAHADHARI


 Mtakwimu mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa akiongea na wandishi wa habari (hawapo pichani)Leo Jijini Dodoma kuhusu utapeli unaofanywa Kwa njia ya mtandao kuhusu kuwepo kwa nafasi za kazi za makarani jambo ambalo amelikanusha

*****

Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog-DODOMA

OFISI ya Taifa ya Takwimu(NBS)na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(OCGS),zote kwa pamoja zimetoa tahadhari kwa wananchi wote kujiepusha na utapeli wa aina yoyote unaohusu ajira kwenye ofisi hizo na kuweka wazi kuwa ofisi hizo bado  hazijatangaza nafasi za kazi za Makarani wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kuonekana kwa tovuti yenye jina la https://www.sensatanzania.com ambayo inatangaza kuwepo kwa nafasi za kazi za makarani wa sensa na tayari baadhi ya watu wameshajisajili kwenye mfumo huo kwa malipo.


Tahadhari hiyo ilitolewa jijini hapa leo na Mtakwimu Mkuu wa Serikali,Dkt.Albina Chuwa wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu taarifa hiyo ambapo aliwata ka  wananchi kutambua kua Serikali haijaanzisha tovuti rasmi ya sensa hivyo tovuti hiyo si rasmi na haitambuliwi na Serikali.


"Nafasi za Ukarani na usimamizi wa sensa zitatangazwa rasmi kupitia tovuti mitandao ya kijamii ya NBS na OCGS,Radio,runinga na magazeti mara baada ya taratibu zote za Serikali zitakapokamilika,"amesema.


Amesema kazi ya kuwapata watumishi hao wa sensa itasimamiwa na kamati za sensa za Mkoa ambazo wenyeviti wake ni wakuu wa mikoa husika.


"Nia ya serikali kufanya hivyo ni kuhakikisha watu wote wanaotaka kufanya kazi za ukarani na usimamizi wa sensa watoke katika maeneo yao wanayoishi,"amesema.


Dkt.Chuwa amesema hadi sasa Ofisi imeshatoa taarifa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)ili wachukue hatua za haraka kuwabaini matapeli wa aina hiyo.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

1 comment:

  1. Aisee mimi nimeibiwa tayari nimetuma ela ya usajili kwa namba hii 0692565395
    Na nikaambiwa ongera mamba yako ya utambulisho ni ST-2022-851579😭😭😭

    ReplyDelete

Pages