WATAHINIWA 11,523 HAWAKUFANYA MTIHANI WA KCPE



Na BENSON MATHEKA

WATAHINIWA 11,523 hawakufanya mtihani wa KCPE mwaka jana licha ya kusajiliwa. Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Profesa Geoge Magoha, japo idadi hiyo ilipungua kutoka 12 424 mwaka wa 2020, serikali itachunguza walikoenda wanafunzi hao.

Hata hivyo, alisema kwamba kaunti 12 zilikuwa na watahiniwa wengi wasichana kuliko wavulana. Kaunti hizo ni Mombasa, Meru, Isiolo, Tharaka Nithi, Nairobi, Uasin Gishu, Busia, Bungoma, Kakamega, Vihiga, Kisumu na Siaya.

Katika KCPE ya mwaka wa 2020 ni kaunti 20 zilizokuwa na wasichana wengi kuliko wavulana katika mtihani huo.

Prof Magoha alisema kwamba hali hii inaonyesha kuwa mtoto mvulana ameanza kuzingatiwa katika masuala ya elimu.

“Kuna dalili kwamba mtoto mvulana ambaye alikuwa ameanza kutelekezwa ameanza kupewa kipau mbele katika masuala ya elimu,” alisema Prof Magoha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments