MICHE ELFU 80 YA PALM TREES KUPANDWA NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA

Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe. Godson Gypson akipanda mti 

Na Mbuke Shilagi - Bukoba

Kamati ya Mladi wa Kuhifadhi Mazingira maarufu kama Palm Tree imeanza kupanda miti ya Palm katika baadhi ya maeneo ya Halimashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Aina hiyo ya miti ya Palm imezinduliwa rasmi kwa kupandwa katika kata ya Bakoba huku zoezi hilo likiongozwa na Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe. Godson Gypson akishirikiana na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Eng. Pasaka Bakari pamoja na Balozi Khamis Sued Kagasheki.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjumbe wa kamati ya Mladi wa Kuhifadhi Mazingira (Palm tree) Bi. Diyana Deus amesema kuwa miche hiyo yote itapandwa katika barabara zote za Manispaa kwa lengo la kuhakikisha Mazingira ya Mji wa Bukoba unapendeza kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri na rafiki kwa miti hiyo.

Aidha Bi. Diyana ameziomba taasisi mbalimbali kujitokeza katika kuleta maendeleo kama alivyofanya Bw. Justine Kimodoi ambaye ni mzaliwa wa Bukoba anayeishi Texas Malekani aliye kuja na wazo la kuipendezesha Bukoba kwa kupanda miti ya Palm.

Huku akisema kuwa kutokana na miche hiyo kuwa na gharama vipo baadhi ya vikundi vinavyojihusisha na uzalishaji wa miche kwa bei elekezi huku akiwataka watumie fursa hiyo kuotesha Miche ya miti hiyo kwa wingi ili iweze kuwaingizia kipato.

Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe. Godson Gypson akipanda mti 
Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe. Godson Gypson akipanda mti 
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba  Mhandisi Pasaka Bakari akipanda mti
Balozi Khamis Kagasheki akipanda mti

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments