WAZIRI MCHENGERWA-RAIS SAMIA AWEKA BILIONI 1 KWENYE MFUKO WA MAENDELEO YA SANAA NA UTAMADUNI

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wadau wa Filamu nchini na kufafanua mafanikio ya Serikali kwenye tasnia hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akizungumza na wadau wa Filamu nchini na kufafanua mafanikio ya Serikali kwenye tasnia hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Wadau mbalimbali wa sanaa wakifuatilia mkutano na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa pamoja na viongozi mbalimbali wa tasnia hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam *************************** NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameweka wazi kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu ana dhamira ya kuboresha na kunyanyua kazi za Sanaa nchini na ameongeza Fedha Kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni. Akizungumza na wadau wa kazi za Sanaa nchini Waziri Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania inatambua Mchango wa kazi za Sanaa nchini na awamu ya 6 imedhamiria kuboresha Miundombinu ya kazi za Sanaa na kwa kuanza Rais ameweka billion 1 kwa Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni. "Dhamira yangu ni kuona Sekta ninazo simamia kuona zinapiga hatua kubwa tunahitaji kufanya Mapinduzi nakuona Maendeleo ya Sanaa ya Filamu nchini hivyo Serikali Ina dhamira pia ya kuhakikisha kazi za Sanaa zinafika mbali na zinakuwa zenye viwango na Mama Samia ameongeza takribani bilioni 1 na kufikia bilioni 2.5 katika Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa hivyo Wasanii wajitokeze kukopa Fedha hizo ." Hata hivyo Mchengerwa ameeleza kuwa Wasanii Wizara itahakikisha wanachapa kazi na hakuna kazi ya Sanaa itakayosimama Kwa kisingizio cha Fedha kwani Milango ipo wazi Kwa wadau wa Filamu kukopesheka Kwa Fedha hizo Ili kuona Kwa namna gani watayarishaji wanatengeneza kazi zenye viwango na Bora zenye kutambulisha Utamaduni wa Taifa la Tanzania. "Ule mkamwo wa kusitasita kutengeneza Filamu zenye uhalisia Sasa basi tayari Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa una shilingi Bilioni 2.5 ni Fedha Kwa ajili ya kazi za Sanaa ambapo Mtayarishaji atakopeshwa Fedha hizo bila malipo ya riba hivyo tunategemea kazi za Sanaa nzuri zitazalishwa Kwa wingi na zenye ubora Ili kufikia Masoko ya nje." Aidha, Mchengerwa ameeleza dhamira nyingine ya wizara yake kuweka Mkakati wa wizara kuwa na televisheni na radio Ili kuweza kuonyesha kazi za Sanaa Kwa masaa 24 na kuwapa fursa Wasanii wanaochipukia kuonekana Pamoja Mkakati wa wizara kuwa na Vyombo vya kisasa vya kuandaa Filamu ambavyo vitakuwa vikikodishwa . Pamoja na hayo Waziri Mchengerwa amewaomba Wasanii kuonyesha ushirikiano na wizara husika na kuahidi kushikamana na wasanii bega Kwa bega na Wasanii kuhakikisha kazi zinajitangaza na kuwaleta watu wenye Mchango katika Sekta ya Filamu kidunia Ili kusaidia kiwanda cha Filamu nchini kinakua na wigo mpana . Mchengerwa ameongeza kuwa Wizara Ina Mkakati wa kujenga nyumba Kwa Wasanii zenye hadhi kwani Serikali inatambua Mchango wa Sanaa nchini katika kutangaza Utamaduni. Kwa upande wake Katibu Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo amebainisha changamoto na Mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia vikao vilivo fanyika Kwa kushirikisha viongozi,Wasanii na wadau wa Filamu na vyama vya Wasanii. "Katika Mafanikio yaliyopatikana kupitia Serikali ya Jamhuri wa Tanzania Kwa kushirikiana na bodi ya Filamu nchini tuliweza kushirikisha vyama vya Wasanii , Wasanii na wadau na tukagundua vitu mbalimbali ikiwemo swala la kupatiwa Tuzo kama kielelezo Cha kutambua Mchango wa kazi za Sanaa na 2021 tuliweza kufanikiwa kuwepo Kwa Tuzo za Sanaa". Aidha Dkt.Kilonzo ameongeza kuwa mbali na kuwepo Kwa Tuzo kulihitajika Mitaji Kwa ajili ya kuongeza ubora wa kazi zao pamoja na changamoto ya Kodi na tozo Kwa Filamu. Pia amebainisha baadhi ya Mafanikio yaliyopatikana ikiwemo Filamu mbili "Vuta nikuvute" na Filamu ya "Binti" kushinda Tuzo pamoja na Kuonyeshwa katika Mtandao wa Kimataifa wa kuonyesha Filamu Netflix.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments