STANSLAUS NYONGO AJITOSA KUWANIA KITI CHA NAIBU SPIKA


Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo akionesha kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) fomu ya kuomba ridhaa kuwania kiti cha Naibu Spika ambapo ameahidi kuwa iwapo atachaguliwa atakuwa kiongozi mwema.

 Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog - DODOMA.

Mbunge wa Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo amefika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiongea leo Februari 6,2022 na Waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu amesema amefikia uamuzi huo kwa kuwa ana sifa nyingi za ziada zinazomtambulisha kwenye masuala ya uongozi.

"Natambua kuwa naweza kuongoza nafasi hii,mbali na ubunge nina sifa nyingi za ziada zinazonifanya nishawishike kuchukua fomu kutetea nafas hii ,"amesema.

Mbunge huyo wa Maswa Mashariki ametumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wake wa Chama kumuamini na kwamba ana matarajio makubwa katika kuwatumikia wananchi na Serikali.

"Endapo nitaipata nafasi hii,nitaitumia vizuri kuishauri Serikali ili kuleta manufaa kwa wananchi,tunatambua kuwa wananchi wa pembezoni wanahitaji Bunge liishauri vizuri Serikali ili wapate kuboreshewa huduma zote za msingi na kuwa na unafuu wa maisha mazuri,"amefafanua Mbunge huyo.


Mbali na kuwa mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Nyongo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa madini kwa Serikali ya awamu ya tano na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii anayoitumikia hadi sasa.
Mbunge wa Maswa mashariki Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ofisi ya Itikadi na Oganaizesheni ya CCM Jijini Dodoma.

Mbunge wa Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo akiongea na Waandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania kiti cha Naibu Spika wa Bunge.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments